Tangazo la Ajira – PSRS
Ofisi ya Rais – Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
Kumb. Na. JA.9/259/01/B/143
Tarehe: 25 Machi, 2025
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Taasisi ya Maji (Water Institute – WI), Taasisi ya Uhasibu Tanzania (Tanzania Institute of Accountancy – TIA), Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania (Tanzania Library Services Board – TLSB), Baraza la Mitihani la Taifa (National Examinations Council of Tanzania – NECTA), Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (Higher Education Students’ Loans Board – HESLB) na Taasisi ya Ardhi Morogoro (Ardhi Institute Morogoro – ARIMO), inakaribisha maombi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi hamsini na saba (57) za kazi kama zilivyoainishwa hapa chini.
Taasisi Zinazotangaza Nafasi za Kazi
- Water Institute (WI)
- Tanzania Institute of Accountancy (TIA)
- Tanzania Library Services Board (TLSB)
- National Examinations Council of Tanzania (NECTA)
- Higher Education Students’ Loans Board (HESLB)
- Ardhi Institute Morogoro (ARIMO)
Sifa za Waombaji
- Mwombaji awe raia wa Tanzania
- Awe na elimu, uzoefu na ujuzi unaolingana na nafasi inayotangazwa
- Awe na umri unaoendana na masharti ya ajira husika
- Awe na uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi ndani ya taasisi za umma
Jinsi ya Kutuma Maombi
Waombaji wenye sifa wanatakiwa kuwasilisha maombi yao kupitia mfumo wa Ajira Portal unaopatikana kupitia tovuti rasmi ya Sekretarieti ya Ajira:
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe (tarehe ya mwisho kuwekwa kulingana na tangazo rasmi).
Kwa maelezo zaidi kuhusu sifa za kila nafasi na maelekezo ya kutuma maombi, tafadhali tembelea tovuti ya Ajira Portal.
Leave a Comment