Nafasi za Kazi 21 Kutoka Utumishi (MDAs & LGAs) 2025

0
Nafasi 21 za Kazi Kutoka Utumishi (MDAs & LGAs) 2025

Nafasi za Kazi 21 Mpya Utumishi 2025: Accountants na Nahodha Watafutwa

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi ishirini na moja (21) katika Wizara, Idara, Wakala za Serikali na Mamlaka za Serikali za Mitaa (MDAs & LGAs).

Accountant II – Mhasibu Daraja la II (Nafasi 20)

Majukumu ya Kazi

  • Kuandika taarifa ya mapato na matumizi
  • Kuandika taarifa za maduhuli
  • Kupokea maduhuli ya serikali na kupeleka Benki kwa wakati
  • Kufanya usuluhisho wa hesabu za Benki
  • Kukagua hati za malipo
  • Kufanya kazi nyingine za fani ya Uhasibu

Sifa za Mwombaji

  • Shahada ya Uhasibu/ Biashara (iliyobobea Uhasibu) au
  • Stashahada ya Juu ya Uhasibu kutoka Taasisi inayotambuliwa na Serikali
  • Cheti cha CPA(T) au sifa inayolingana inayotambuliwa na NBAA

Ngazi ya Mshahara

  • TGS E

Skipper II – Nahodha Daraja la II (Nafasi 1)

Majukumu ya Kazi

  • Kubuni na kuunda zana za kuvulia samaki
  • Kutunza na kutengeneza zana za kuvulia
  • Kuendesha boti ndogo za futi 40 zenye tani 50–200 (GRT)
  • Kushiriki shughuli za uvuvi katika boti/meli

Sifa za Mwombaji

  • Stashahada ya Unahodha na Uvuvi kutoka Chuo cha Uvuvi Mbegani au kinachotambuliwa na Serikali

Ngazi ya Mshahara

  • TGS C

Masharti ya Jumla kwa Waombaji

  • Awe raia wa Tanzania mwenye umri usiozidi miaka 45 (isipokuwa walioko kazini Serikalini)
  • Wenye ulemavu wanahimizwa kuomba na kuainisha aina ya ulemavu
  • Wambatishe cheti halali cha kuzaliwa kilichothibitishwa
  • Wasilishe C.V yenye maelezo ya kina na majina ya wadhamini watatu
  • Wambatishe vyeti vya taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili
  • Testmonials, Provisional Results, Statement of Results, na result slips za kidato cha nne/sita HAZITAKUBALIWA
  • Waliosoma nje ya nchi wahakikishe vyeti vimeidhinishwa na TCU, NECTA, au NACTE
  • Waliostaafu bila kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi hawaruhusiwi kuomba
  • Walioko serikalini katika nafasi za kuingilia wasitumie nafasi hizi
  • Watakaotoa taarifa za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria

Mwisho wa Kutuma Maombi

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here