Ajira Mpya Kahama Municipal Council Mei 2025
Halmashauri ya Manispaa ya Kahama imetangaza nafasi mpya za ajira kwa mwaka wa fedha 2024/2025, kufuatia kibali cha ajira kutoka Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kilichotolewa tarehe 29 Aprili 2025. Watanzania wenye sifa wanakaribishwa kutuma maombi kuanzia Mei 14, 2025.
Nafasi Zinazotangazwa:
1. Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja II – Nafasi 04
Sifa za Mwombaji:
- Elimu ya kidato cha nne au sita
- Stashahada (NTA Level 6) katika:
- Utunzaji wa Kumbukumbu
- Urasimu Ramani (Cartography)
- Geo-Informatics
- Sheria
- Kumbukumbu za Afya
- Ujuzi wa matumizi ya kompyuta kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali
Majukumu:
- Kuorodhesha barua zinazoingia na kutoka
- Kusambaza na kupokea majalada
- Kutafuta na kurudisha kumbukumbu
- Kufuatilia mzunguko wa majalada
Mshahara: Kwa mujibu wa ngazi ya serikali ya TGS C1
2. Dereva Daraja II – Nafasi 03
Sifa za Mwombaji:
- Elimu ya kidato cha nne au sita (kuanzia daraja la nne)
- Mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari kutoka VETA, NIT au chuo kinachotambuliwa na serikali
- Leseni ya daraja C au E
- Awe mwadilifu na hajawahi kutiwa hatiani
Majukumu:
- Kukagua usalama wa gari
- Kuwasafirisha watumishi
- Kusambaza nyaraka
- Kuhifadhi taarifa za safari
- Kufanya usafi wa gari
Mshahara: Kwa mujibu wa ngazi ya serikali ya TGS B1
Masharti ya Jumla kwa Waombaji Wote:
- Awe Mtanzania mwenye umri kati ya miaka 18 hadi 45
- Ambatanisha nakala ya cheti cha kuzaliwa
- Ambatanisha C.V yenye taarifa binafsi na namba za simu
- Ambatanisha vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa na wakili au Kamishna wa viapo
- Vyeti vya nje ya nchi lazima vifanyiwe ulinganishi na TCU au NACTE
- Ambatanisha picha moja ya “passport size” ya hivi karibuni
- Maombi yaandikwe kwa Kiswahili au Kiingereza na yasainiwe
Jinsi ya Kutuma Maombi:
Tuma maombi kupitia Mfumo wa Kielektroniki wa Ajira kwa anuani:
🔗 https://portal.ajira.go.tz
Anuani ya barua:
Mkurugenzi wa Manispaa,
Barabara ya Boma,
S.L.P 472,
KAHAMA – Shinyanga.
⚠️ Maombi yatakayowasilishwa nje ya mfumo huu hayatazingatiwa.
🗓 Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 27 Mei, 2025. Usikose fursa hii ya kujiunga na Manispaa ya Kahama.
Leave a Comment