Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya 2023/24, Stephenie Aziz Ki, amefafanua kuwa baada ya kila mchezo, maandalizi yanaelekezwa kwenye mchezo unaofuata.
Yanga SC walijipanga Afrika Kusini walipoalikwa kushiriki mashindano maalumu na kushinda Kombe la Toyota kwa mabao 4-0. Katika mchezo huo, Aziz Ki alifunga mabao mawili, Clement Mzize alifunga moja, na Prince Dube alifunga bao la ufunguzi.
Agosti 4, 2024, Yanga walisherehekea Wiki ya Wananchi kwa kushinda Red Arrows 2-1 katika mchezo wa kimataifa, ambapo Aziz Ki alifunga bao moja.
Aziz Ki alisema: “Kila baada ya mchezo, tunatazamia kile kinachofuata. Tulicheza na Red Arrows kwenye Ngao ya Jamii, lakini sasa tunazingatia maandalizi mazuri ili kufanya vizuri kwenye mchezo unaokuja.”
Leave a Comment