Michezo

Mudathir Yahya Aendeleza Moto Yanga SC

Mudathir Yahya Aendeleza Moto Yanga SC

Mwanasoka mahiri Mudathir Yahya ameonyesha tena uwezo wake wa hali ya juu katika msimu wa 2024/25. Kulingana na Maulid Kitenge, kiungo huyu wa Yanga ataendelea kufanya maajabu na kuwasha moto dimbani.

Agosti 4, katika tukio la utambulisho wa wachezaji wapya na wale waliokuwepo msimu wa 2023/24 kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi, Mudathir alifunga bao moja muhimu kwenye ushindi wa Yanga 2-1 dhidi ya Red Arrows.

Dakika ya 64, aliweka usawa kwa kufunga bao lililosawazisha la Red Arrows lililofungwa kipindi cha kwanza na Ricky Banda dakika ya 5. Bao la ushindi la Yanga lilifungwa na Stephane Aziz Ki dakika ya 90 kwa mkwaju wa penalti baada ya Nickson Kibabage kufanyiwa faulo na beki wa Red Arrows.

Maulid Kitenge alisema, “Kwa muda simu zitaita sana kwa kuwa msimu uliopita ziliita ni mwendelezo wa furaha.”

Wiki ya Mwananchi ilivunja rekodi kwa kujaza mashabiki wengi katika viwanja viwili kwa wakati mmoja. Uwanja wa Mkapa ulijaa hadi kufurika huku Uwanja wa Uhuru pia ukiwa na mashabiki wa Yanga waliojitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hilo la sita kwa Yanga.

Msimu wa 2024/25 unaonyesha kuwa wa kuvutia zaidi kwa mashabiki wa Yanga, huku Mudathir Yahya akiendelea kung’ara dimbani.

Leave a Comment