Mechi za Leo Zitaamua Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika 2025

0
Mechi za Leo Zitaamua Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika 2025

Mechi za Uamuzi za Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika 2025

Timu Zitakazocheza Fainali Kupatikana Leo

Baada ya mechi za kwanza za hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kumalizika kwa sare tasa, hatima ya timu zitakazocheza fainali inatarajiwa kujulikana leo jioni.

Mchezo wa kwanza utafanyika saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Cairo, ambapo Al Ahly ya Misri itakipiga dhidi ya Mamelodi Sundowns kutoka Afrika Kusini.

Mchezo wa Pili: Pyramids vs Orlando Pirates

Saa mbili baadaye, Pyramids FC itawakaribisha Orlando Pirates kwenye Uwanja wa Juni 30, jijini Cairo. Hii ni mechi nyingine muhimu ambayo itaamua ni timu gani itaingia fainali.

Muda wa Kuamua Nani Anaenda Fainali

Kwa kuwa mechi za awali ziliisha kwa sare bila mabao, timu zote zinahitaji ushindi ili kufuzu. Wenyeji wanahitaji pointi zote tatu, lakini wageni wanaweza kusonga mbele kwa ushindi au sare yenye mabao. Endapo sare tasa itajirudia, washindi wataamuliwa kwa mikwaju ya penalti.

Kauli za Makocha Kabla ya Mechi

Marcel Kohler – Al Ahly

Kocha wa Al Ahly, Marcel Kohler, amesema kuwa wamejiandaa kikamilifu na amewataka mashabiki wajitokeze kwa wingi kuisapoti timu.

“Katika mechi ya kwanza, hakuna timu iliyofunga, hivyo tunatarajia ushindani mkali. Tuko nyumbani mbele ya mashabiki wetu. Tunahitaji sapoti yao kuanzia dakika ya kwanza hadi mwisho,” alisema Kohler.

Miguel Cardoso – Mamelodi Sundowns

Kocha wa Sundowns, Miguel Cardoso, amesema kuwa timu yake haina hofu ya kucheza mbele ya mashabiki wa Al Ahly na wanatarajia kupata matokeo chanya.

“Tunapozomewa ugenini, huwa tunajua tunafanya vizuri. Hilo ndilo tunaloishi – kucheza bila woga, kwa shauku,” amesema Cardoso.

Mechi hizi mbili za nusu fainali ni fursa kwa timu nne kutafuta tiketi ya kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika 2025. Mashabiki wanatarajia burudani ya hali ya juu na ushindani mkali uwanjani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here