Mchambuzi wa soka kutoka Crown Media, Geoff Lea, ametoa maoni yake kuhusu msimu wa Ligi Kuu Tanzania wa 2024/25, akitabiri kuwa Klabu ya Yanga ina nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa tena.
“Kwa msimu huu wa 2024/25, mpinzani mkubwa wa Yanga ni Azam FC na sio Simba. Kuhusu nafasi za kutwaa ubingwa, naipa Yanga asilimia 50%, Azam 30%, na Simba 20%. Simba bado inajengwa, hivyo hawawezi kubeba ubingwa msimu huu,” amesema Geoff Lea.
Leave a Comment