Mayele Afunga Mbili Aisaidia Pyramids Kutinga Fainali Ligi ya Mabingwa
Mayele Aibeba Pyramids kwa Mabao Mawili
Fiston Kalala Mayele ameonesha ubora wake kwa kufunga mabao mawili muhimu na kuisaidia Pyramids FC kutinga fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) baada ya ushindi wa jumla wa 3-2 dhidi ya Orlando Pirates katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Juni 30, Cairo.
Mafarao Wapindua Wasauzi
Katika mechi iliyosheheni ushindani, matumaini ya kuwa na fainali ya Wasauzi tupu yalifutika baada ya Pyramids kuonyesha uimara wao dhidi ya Pirates. Hivyo sasa, Pyramids watakutana na Mamelodi Sundowns kwenye fainali ya CAFCL.
Matokeo ya Mechi (Aggregate 3-2)
- ⚽ 41’ Mofokeng (Orlando Pirates)
- ⚽ 45+1’ Mayele (Pyramids)
- ⚽ 52’ Nkota (Orlando Pirates)
- ⚽ 57’ Sobhi (Pyramids)
- ⚽ 84’ Mayele (Pyramids)