Matokeo ya Yanga Vs Simba: Nani Ataibuka Kidedea Ngao ya Jamii?
Matokeo ya Yanga dhidi ya Simba Ngao ya Jamii 08/08/2024 | Mechi ya Ngao ya Jamii 2024
Yanga Sc | 1 – 0 | Simba Sc |
Mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara mara tatu mfululizo, Yanga SC, wanakutana leo na mabingwa watetezi wa Ngao ya Jamii, Simba SC, katika nusu fainali ya Ngao ya Jamii ya msimu wa 2024. Mechi hii itafanyika Agosti 08, 2024, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, kuanzia saa moja usiku. Timu hizi zimekutana mara tisa katika michuano hii, Simba wakiwa washindi mara tano na Yanga mara nne. Mwaka jana, Simba walishinda kwa mikwaju ya penalti baada ya sare tasa.
Yanga, inayonolewa na kocha Miguel Gamondi, inatazamia kulipiza kisasi na kudhihirisha ubora wao dhidi ya Simba licha ya kufanya hivyo katika michezo ya ligi ya msimu uliopita. Gamondi amesisitiza kuwa kipaumbele chake ni Ligi Kuu na michuano ya kimataifa, lakini ushindi dhidi ya watani wao wa jadi utakuwa ni mwanzo mzuri wa msimu.
Simba, chini ya kocha mpya Fadlu Davids, wanakabiliwa na shinikizo la kutetea taji lao na kuendeleza utawala wao katika soka la Tanzania. Davids, aliyerithi mikoba ya Abdelhak Benchikha, anajua umuhimu wa mechi hii kwa mashabiki na uongozi wa Simba.
Wachezaji wapya wa Simba kama mshambuliaji hatari Debora Fernandez, Jean Charles Ahoua, na Mutale wanatarajiwa kuleta mabadiliko makubwa. Yanga nao wameimarisha kikosi chao kwa usajili wa wachezaji wenye uzoefu kama Prince Dube.
Matokeo ya Yanga Vs Simba Leo Ngao Ya Jamii 08/08/2024
Hapa chini tutakuletea matokeo ya mechi ya Yanga dhidi ya Simba Ngao ya Jamii 2024:
Yanga SC π Simba SC
- π Ngao ya Jamii πΉπΏ
- β½οΈ Young Africans SC πΉπΏπSimba SC πΉπΏ
- π 08.08.2024
- π Uwanja wa Benjamin Mkapa
- π Saa Moja Usiku πΉπΏ
Leave a Comment