Michezo

Matokeo ya Simba Vs APR Leo – Simba Day 2024

Matokeo ya Simba Vs APR Leo - Simba Day 2024

Matokeo Ya Simba Day Leo vs APR

Klabu ya Simba leo inachuana na APR FC kwenye mchezo wa kirafiki unaoadhimisha Simba Day. Mchezo huu unafanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 88 tangu kuanzishwa kwa klabu hiyo yenye makazi yake Kariakoo, Ilala.

Matokeo ya Simba Vs APR Leo 03 Agosti 2024 – Simba Day

Simba SC2 – 0APR FC
Matokeo ya Simba Vs APR Leo Highlights VIDEO

First Half

  • Dakika 20 za mchezo zimepita bila kufungana: Simba 0-0 APR FC
  • Dakika ya 43, Simba wanapata penati baada Mutale kuchezewa faulo kwenye boksi
  • Mkwala anakosa penati. Dakika ya 44 Simba 0-0 APR FC

Second Half

  • Dakika ya 46 Debora Fernandez anaifungia Simba goli la kuongoza
  • Dakika ya 66 Balua anaifungia Simba goli la pili

APR FC: Mabingwa wa Rwanda Wawasili Tanzania

APR FC, mabingwa wa Ligi Kuu ya Rwanda, waliwasili Dar es Salaam asubuhi ya Ijumaa, Agosti 2, wakiwa na kikosi cha wachezaji 24, wakiwemo wachezaji wapya 10 kama Lamine Bah kutoka Mali na Wanigeria Johnson na Odibo. Baadhi ya wachezaji muhimu waliokosa safari ni Nshimirimana Ismael Pichou, Apam Bemol, na Kwitonda Alain Bacca.

Simba SC: Kujipima Nguvu Dhidi ya Mabingwa wa Rwanda

Hii ni fursa muhimu kwa APR FC kujipima nguvu dhidi ya timu kubwa kama Simba kabla ya mechi yao ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Azam FC itakayofanyika Agosti 18. Ingawa ni mchezo wa kirafiki, mashabiki wanatarajia ushindani mkubwa huku kila timu ikijaribu kuonyesha uwezo wao na kuwafurahisha mashabiki.

Matokeo ya Simba Vs APR Leo - Simba Day 2024
Matokeo ya Simba Vs APR Leo – Simba Day 2024

Simba Day: Sherehe ya Utamaduni na Mpira

Simba Day ni tukio kubwa linalofanyika kila mwaka na kuvuta maelfu ya mashabiki. Mwaka huu, zaidi ya mashabiki 60,000 wanatarajiwa kujaza uwanja wa Benjamin Mkapa. Sherehe za Wiki ya Simba zilianza Julai 24, zikiambatana na shughuli za kijamii kama michango ya damu na misaada kwa wenye mahitaji maalum, kuonyesha kujali jamii.

Kabla ya Simba Day, Simba walikuwa na mechi za kirafiki nchini Misri, wakijaribu kuboresha kikosi chao kwa ajili ya msimu mpya. Msimu uliopita, Simba walikumbana na changamoto nyingi, wakitolewa kwenye robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Al Ahly, na kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Matumaini ya Simba kwa Msimu Mpya

Simba inatarajia mafanikio makubwa msimu ujao kutokana na maandalizi makubwa na usajili mpya wa wachezaji. Simba Day itakuwa fursa ya kutambulisha wachezaji wapya na kuimarisha mshikamano kati ya klabu na mashabiki wake. Mashabiki wa Simba wanasubiri kwa hamu kuona timu yao ikirejea kwenye ubora wake na kufanikiwa katika mashindano ya ndani na nje ya nchi.

Leave a Comment