Michezo

Matokeo ya Kaizer chiefs Vs Yanga Leo – Toyota Cup

Matokeo ya Kaizer chiefs Vs Yanga Leo – Toyota Cup

Matokeo ya Kaizer chiefs Vs Yanga Leo 28/07/2024 | Matokeo ya Yanga Dhidi ya Kaizer chiefs Leo | Yanga Vs Kaizer

Leo ni siku ya kihistoria kwa mashabiki wa soka Tanzania na Afrika Kusini! Timu ya Wananchi, Yanga Sc, wanakutana uso kwa uso na Kaizer Chiefs katika uwanja wa Toyota Stadium, Bloemfontein majira ya saa tisa alasiri kwa masaa ya Afrika kusini na saa kumi jioni kwa masaa ya Tanzania. Huu ni mchuano wa kwanza kabisa wa Toyota Cup, mashindano mapya yanayoanza kuchanua katika anga la soka Afrika.

Mechi hii imebeba uzito mkubwa kutokana na ubora wa timu zote mbili. Yanga Sc, mabingwa wa ligi kuu na Kombe la Shirikisho Tanzania, wamewekeza katika usajili wa wachezaji mahiri, na tayari wameonyesha makali yao katika mashindano ya Mpumalanga Premiers International Cup 2024. Kaizer Chiefs, wakiwa chini ya kocha mpya Nasreddine Nabi, wanatafuta kuonyesha kwamba wamebadilika na wako tayari kurejea kwenye kiwango chao cha juu kama ilivozoeleka katika historia ya soka Afrika kusini.

Matokeo ya Kaizer chiefs Vs Yanga Leo 28/07/2024 – Toyota Cup

Kaizer chiefs0 – 4Yanga

Kipindi cha Kwanza Kimemalizika; Kaizer Chiefs 0-2 Yanga Sc

  • Dakika 25, Dube anaipa Yanga Goli la kuongoza
  • Dakika 47, Aziz Ki anaipa Yanga Goli la pili

Kipindi cha Pili Kimeanza: Kaizer Chiefs 0-2 Yanga Sc

  • Dakika Ya 57 Mzize anaipa Yanga goli la 3
  • Dakika Ya 63 Aziz Ki anatupia goli lake la pili na goli la 4 kwa Yanga

Taarifa Kuhusu Mechi ya Yanga Vs Kaizer Chiefs

  • ToyotaCup
  • Kaizer Chiefs vs. Young Africans SC
  • First Team
  • Jumapili 28 Julai 2024
  • Toyota Stadium, Bloemfontein
  • 15h00
Matokeo ya Kaizer chiefs Vs Yanga Leo – Toyota Cup
Matokeo ya Kaizer chiefs Vs Yanga Leo – Toyota Cup

Maandalizi ya Mechi na Matokeo ya Pre-Season

Kaizer Chiefs wamekuwa na maandalizi mazuri katika kambi yao ya Uturuki, wakishinda mechi kadhaa za kirafiki, ikiwa ni pamoja na ushindi mnono wa 5-2 dhidi ya Al Shahaniya ya Qatar. Hata hivyo, mechi hii ya leo itakuwa tofauti, ikichezwa mbele ya mashabiki wengi wenye shauku.

Yanga Sc pia wako katika kiwango bora, wakiwa wametoka kushinda mechi yao ya hivi karibuni kwa kuonyesha soka la kuvutia.

Leave a Comment