Michezo

Matokeo ya Azam Vs Coastal Union Leo Ngao ya Jamii, Agosti 8

Matokeo ya Azam Vs Coastal Union Leo Ngao ya Jamii, Agosti 8

Matokeo ya Azam Vs Coastal Union Leo Ngao ya Jamii 08/08/2024 | Matokeo ya Azam fc Dhidi ya Coastal Union Leo

Klabu ya Azam Fc leo itakutana na Coastal Union katika mchezo wa kwanza wa michuano ya Ngao ya jamii ambao umepangwa kuchezeka katika uwanja wa Amaan, Zanzibar leo saa 10 jioni.

Mchezo huu unatarajiwa kua wenye ushindani mkubwa kutokana na maandalizi ambao pande zote mbili wamefanya katika kipindi hichi ambapo vilabu hivi vilikua katika kambi maalumu za kujiandaa na msimu mpya.

Matokeo ya Azam Vs Coastal Union Leo Ngao ya Jamii

Azam Fc5 – 2Coastal Union

Timu zote mbili zimekuwa katika maandalizi maalumu kwa muda sasa, zikijipanga kuhakikisha zinaanza msimu mpya kwa nguvu. Azam FC na Coastal Union, zote zimeweka kambi na kufanya mazoezi ya nguvu kuhakikisha kuwa zinaingia kwenye mchezo huu zikiwa tayari kwa ushindani. Timu hizi zimekutana mara kadhaa katika michezo ya kirafiki na ya mashindano, na kila mara zimekuwa zikitoa ushindani mkubwa, jambo linalotarajiwa pia kutokea leo.

Kila timu ina wachezaji nyota ambao huenda wakawa na uamuzi mkubwa katika matokeo ya mchezo huu. Coastal Union inamtegemea kipa Ley Matampi, aliyeshinda tuzo ya kipa bora wa Ligi Kuu msimu uliopita, pamoja na kiungo Charles Semfuko na mawinga hatari Hassan Abdallah na Denis Madzaka.

Azam FC, kwa upande wao, wanamtegemea mshambuliaji wao mpya Jhonier Blanco, ambaye ameonyesha makali yake katika mechi za kujipima nguvu. Viungo Feisal Salum na Jibril Sillah, ambao walikuwa na msimu mzuri uliopita, pia watakuwa muhimu katika kuunda nafasi za mabao. Kipa Mohamed Mustafa, aliyesajiliwa hivi karibuni, anatarajiwa kuimarisha safu ya ulinzi ya Azam FC.

Makocha wa pande zote mbili wamekiri ugumu wa mchezo huu. David Ouma wa Coastal Union amesema kuwa wanajipanga kukabiliana na Azam FC kama timu, huku Bruno Ferry wa Azam FC akisisitiza umuhimu wa kupata ushindi ili kuingia fainali.

  • 🚨 M A T C H D A Y 🚨
  • Azam Fc 🆚 Coastal Union
  • 🏆 Community Shield 2024
  • ®️ Semi Final
  • 🏟 New Amaan Complex
  • 🕰 4.00 PM (E.A.T)

Leave a Comment