Matokeo Simba Vs Telecom Egypt leo 28/07/2024 – Mechi ya Kirafiki
Leo, tarehe 28 Julai 2024, mashabiki wa soka wanatarajia kwa hamu mtanange wa kirafiki kati ya wekundu wa Msimbazi, Simba Sports Club, na timu ya Telecom Egypt. Mechi hii itafanyika kwenye uwanja wa Mercure, ikianza saa 1 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Maandalizi ya Simba SC kwa Msimu Mpya
Mechi hii ni sehemu muhimu ya maandalizi ya Simba SC kuelekea msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara unaotarajiwa kuanza tarehe 8 Agosti. Wekundu wa Msimbazi wanatumia mchezo huu kujaribu wachezaji wao wapya waliosajiliwa na mbinu mpya za ushindi kabla ya kukutana na wapinzani wao wa jadi, Yanga SC, katika mchezo wa ngao ya jamii.
Huu ni mchezo wa pili wa kirafiki kwa Simba katika kipindi hiki cha maandalizi. Katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya El-Qanah ya Misri, Simba ilionyesha uwezo mkubwa kwa kushinda magoli 3-0. Jean Charles Ahoua alifunga magoli mawili ya haraka, huku Okejepha akifunga goli la tatu na la mwisho katika dakika za nyongeza.
Kikosi na Mbinu za Simba SC
Mashabiki wa soka wanatarajia kuona jinsi Simba itakavyocheza dhidi ya Telecom Egypt. Kocha mpya wa Simba, Fadlu Davids, anatarajia kutumia mechi hii kujaribu mbinu zake za mchezo kabla ya mechi muhimu dhidi ya Yanga SC. Hii itasaidia kutambua maeneo yanayohitaji kuboreshwa. Mechi hii itawapa nafasi wachezaji wapya wa Simba kuonyesha vipaji vyao na kujenga muunganiko mzuri na wachezaji wa zamani. Kuwapa nafasi wachezaji wapya ni muhimu katika kuhakikisha wanaelewana vizuri na wenzao kabla ya kuanza kwa msimu mpya.
Kikosi rasmi cha Simba kitatangazwa muda mfupi kabla ya mechi kuanza. Mashabiki wanasubiri kwa hamu kuona ni akina nani watakaopata nafasi ya kucheza leo. Habariforum tutakuletea taarifa kamili kuhusu kikosi cha Simba leo hapa Kikosi cha Simba Vs Telecom Egypt
Matokeo Simba Vs Telecom Egypt leo 28/07/2024
Telecom Egypt | Vs | Simba Sc |
Leave a Comment