Matokeo Manchester City vs Arsenal Leo – Premier League
Katika mchezo wa leo wa Premier League kati ya Manchester City na Arsenal, mambo yalikua moto uwanjani. Mechi ilianza kwa kasi huku timu zote zikiweka juhudi kubwa kupata matokeo mazuri.
Manchester City | 2 – 2 | Arsenal |
Dakika 9: Manchester City 1 – 0 Arsenal
Mchezo ulianza kwa Manchester City kupata goli la kwanza kupitia kwa Erling Haaland baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Savinho, na kuweka timu yake mbele kwa bao moja.
Dakika 22: Manchester City 1 – 1 Arsenal
Arsenal walirejea kwenye mchezo dakika ya 22 baada ya Riccardo Calafiori kufunga bao la kusawazisha kwa kupokea mpira kutoka kwa Gabriel Martinelli. Mchezo ukawa sare.
Dakika 45 + 1: Manchester City 1 – 2 Arsenal
Hadi mapumziko, Arsenal walikuwa wameongeza bao la pili dakika ya mwisho wa kipindi cha kwanza. Gabriel Magalhães alifunga bao baada ya krosi nzuri kutoka kwa Bukayo Saka, na kufanya matokeo kuwa 1-2 kwa faida ya Arsenal.
Dakika 90 + 8: Manchester City 2 – 2 Arsenal
Katika dakika za majeruhi, John Stones wa Manchester City alifunga bao la kusawazisha na kufanya matokeo ya mwisho kuwa 2-2, na kuacha timu zote zikitoka sare katika mchezo huo wa kusisimua.
Man City vs Arsenal Leo
Mchezo wa leo kati ya Manchester City na Arsenal ulionyesha takwimu zifuatazo:
Takwimu za Mechi: Manchester City vs Arsenal Leo
- Mashuti yaliyolenga lango: Manchester City 10 – 2 Arsenal
- Mashuti nje ya lango: Manchester City 9 – 2 Arsenal
- Mashuti yaliyoblockiwa: Manchester City 11 – 0 Arsenal
- Umiliki wa mpira (%): Manchester City 77% – 23% Arsenal
- Piga kona: Manchester City 6 – 2 Arsenal
- Offsides: Manchester City 0 – 1 Arsenal
- Makosa: Manchester City 6 – 10 Arsenal
- Kupiga mipira nje (Throw-ins): Manchester City 20 – 5 Arsenal
- Kadi za njano: Manchester City 3 – 3 Arsenal
- Kadi nyekundu: Manchester City 0 – 1 Arsenal
- Mipira ya krosi: Manchester City 25 – 8 Arsenal
- Uokoaji wa kipa: Manchester City 0 – 9 Arsenal
- Goal kicks: Manchester City 3 – 12 Arsenal
Hitimisho
Mchezo huu ulikuwa na msisimko mkubwa, huku Manchester City wakionekana kumiliki mpira zaidi lakini Arsenal walipambana kufa na kupona, hadi kufanikisha sare ya 2-2. Manchester City vs Arsenal Leo
Leave a Comment