Baada ya kutambulishwa rasmi FCA Darmstadt ya Ujerumani, straika wa Kitanzania Athuman Masumbuko ‘Makambo Jr’ amecheza mchezo wake wa kwanza wa ligi, akitumika kwa dakika 20 dhidi ya FC Germania. Mechi hiyo ilichezwa kwenye Uwanja wa Sportplatz Rödermark-Ober Roden, ambapo timu ya Makambo ilishindwa kwa mabao 2-1.
Klabu hiyo, anayochezea kijana huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar na Mashujaa FC, inashiriki ligi ngazi ya 7 nchini Ujerumani maarufu kama ‘Gruppenliga’.
Makambo Jr alisema kuwa ingawa ligi hiyo ni ya daraja la chini, muda aliocheza umeonyesha kuwa atahitaji juhudi za ziada kuonyesha uwezo wake na kuaminiwa kikosini. “Dakika chache nilizocheza zilionekana kama mechi mbili kamili. Kasi ya mchezo hapa ni kubwa sana, hakuna muda wa kupumzika. Ligi ni ngumu na inahitaji ukomavu mkubwa. Niliandaa sana Tanzania, lakini naona kuna kazi zaidi mbele yangu,” alisema Makambo Jr.
Leave a Comment