Elimu

Majina ya Waliopata Mkopo HESLB 2024/2025 Awamu Ya Tatu

Majina ya Waliopata Mkopo HESLB 2024/2025 Awamu Ya Tatu

Majina ya Waliopata Mkopo HESLB 2024/2025 Awamu Ya Tatu

Wanafunzi 19,345 Wapangiwa Mikopo ya TZS 59.49 Bilioni Awamu ya Tatu

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza majina ya wanafunzi 19,345 waliopata mkopo kwa Awamu ya Tatu (Batch Three) kwa mwaka wa masomo wa 2024/2025. Kiasi cha mikopo kinachotolewa kwa wanafunzi hawa ni TZS 59.49 bilioni, na wanafunzi wote ni wa shahada za awali (Bachelor Degrees), ambao wamejiunga na taasisi mbalimbali za elimu ya juu nchini.

Idadi ya Wanafunzi Wanaopata Mikopo Yafikia 70,990

Kwa kuongezwa kwa wanafunzi wa Awamu ya Tatu, jumla ya wanafunzi wa shahada ya awali waliopangiwa mikopo kwa mwaka 2024/2025 imefikia 70,990. Thamani ya jumla ya mikopo hii ni TZS 223.3 bilioni. Kati ya wanafunzi hawa, wanaume ni 40,164 (56.58%) na wanawake ni 30,825 (43.42%).

Mikopo kwa Wanafunzi wa Stashahada

Mbali na wanafunzi wa shahada za awali, HESLB pia imetoa mikopo yenye thamani ya TZS 1.1 bilioni kwa wanafunzi wa stashahada. Katika awamu hii, wanafunzi 425 wa stashahada wamepangiwa mikopo, wakiwemo wanafunzi 378 wa mwaka wa kwanza na 47 wanaoendelea na masomo yao.

Ruzuku ya ‘Samia Scholarship’

Mpaka sasa, HESLB imeweza kutoa kiasi cha TZS 3.02 bilioni kwa wanafunzi 599 wanaonufaika na ruzuku ya ‘Samia Scholarship’ kwa mwaka wa masomo wa 2024/2025. Kati ya hawa, wanafunzi 588 walipata ruzuku katika Awamu ya Kwanza, na 11 katika Awamu ya Pili.


Imetolewa na:

Mkurugenzi Mtendaji,
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,
S.L.P. 984,
Dodoma
Jumapili, Oktoba 20, 2024.

Leave a Comment