Taarifa Muhimu kwa Waombaji Kazi Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST)
Uongozi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) kupitia Ofisi ya Makamu Mkuu wa Chuo, unawatangazia waombaji kazi wote kuwa mchakato wa usaili utaanza rasmi kuanzia tarehe 22 Mei 2025.
Usaili huu unalenga kuwapata wagombea wanaofaa kwa nafasi mbalimbali za kazi zilizotangazwa awali, na baada ya zoezi hilo kukamilika, waombaji watakaofaulu watapangiwa vituo vya kazi kulingana na mahitaji ya chuo.
Maelekezo Muhimu kwa Wasailiwa
Waombaji wote walioteuliwa kuhudhuria usaili wanakumbushwa kuzingatia maelekezo yote yaliyowekwa katika orodha ya PDF rasmi. Majina ya walioitwa pamoja na muda na sehemu ya kufanyia usaili vimeainishwa kwa kina katika hati hiyo.
Leave a Comment