Majina ya Walioitwa Mafunzo Jeshi la Zimamoto 2025
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limetangaza rasmi majina ya waombaji waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya Uaskari ngazi ya Konstebo kwa mwaka 2025. Mafunzo haya ni hatua muhimu katika maandalizi ya askari wa zimamoto na uokoaji nchini.
Tarehe na Mahali Mafunzo Yatafanyika
Wote walioitwa wanapaswa kuripoti katika Chuo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kilichopo Chogo, Wilaya ya Handeni, Mkoa wa Tanga, kati ya tarehe 16 hadi 18 Mei 2025. Mtu yeyote atakayeshindwa kufika ndani ya muda huo hatapokelewa, na nafasi yake itatolewa kwa mtu mwingine.
Kwa wanaofika, shuka katika kituo cha Kabuku, ambacho kipo umbali wa kilomita 12 kutoka chuoni. Mapokezi yatafanyika kati ya saa 12 asubuhi hadi saa 4 usiku kwa siku hizo tatu.
Masharti Muhimu kwa Washiriki
Kila mhusika anatakiwa:
- Kujigharamia nauli, chakula na malazi hadi atakapopokelewa chuoni.
- Kuja na vyeti halisi vya masomo, taaluma au ujuzi aliotuma maombi, pamoja na cheti cha kuzaliwa, kitambulisho cha NIDA au namba ya NIDA, na leseni hai kwa madereva.
- Kila cheti kiwe na nakala tatu, na majina katika vyeti vyote lazima yaligane kikamilifu.
- Kupimwa afya ya mwili, akili, na mimba kwa wanawake; yeyote atakayebainika na matatizo ya kiafya hataruhusiwa kuendelea na mafunzo.
Vifaa Muhimu vya Kuambatana Navyo
Washiriki wanapaswa kuja na:
- Mashuka 2 ya bluu, mto 1 na foronya 2 za bluu
- Chandarua cha duara chenye rangi ya bluu
- Ndoo ya plastiki ya lita 20, sahani na kikombe cha bati
- Fedha za matumizi binafsi
- Bima ya afya kwa walio nayo
Pia, vifaa vingine kama raba, T-shirt za bluu, madaftari, vifaa vya michezo (bukta, tracksuit, T-shirt), na kalamu watanunua ndani ya duka la Chuo.
Pakua Orodha ya Majina Waliochaguliwa
Ili kuona majina yote ya walioitwa, tafadhali