MAJINA ya Walioitwa Kazini TFS na TAWA Tarehe 30 Aprili 2025
Tangazo la Matokeo ya Usaili kwa Waombaji Kazi Serikalini
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ametangaza rasmi majina ya waombaji kazi waliofaulu usaili uliofanyika kati ya tarehe 6 Machi hadi 28 Machi 2025. Orodha hii inahusu waombaji walioomba nafasi mbalimbali katika taasisi za Tanzania Forest Services (TFS) na Tanzania Wildlife Management Authority (TAWA).
Majina Yaliyofanikiwa na Kupangiwa Vituo vya Kazi
Orodha iliyotolewa ina majina ya waombaji waliofaulu pamoja na baadhi waliokuwa kwenye kanzidata (Database) ya Sekretarieti, ambao sasa wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.
Waombaji wote waliopangiwa vituo vya kazi wameelekezwa kuingia kwenye akaunti zao za Ajira Portal, kisha kufungua sehemu ya My Applications ili kupakua barua zao za kupangiwa kazi. Baada ya kupakua, wanatakiwa kuchapisha barua hizo na kuzipeleka walikoelekezwa.
Wajibu wa Kuripoti Kazini
Walioitwa kazini wanapaswa kuripoti kwa Mwajiri ndani ya muda uliotajwa kwenye barua za kupangiwa kazi, wakiwa na vyeti halisi vya elimu kuanzia kidato cha nne na kuendelea kwa ajili ya uhakiki kabla ya kupewa barua ya ajira rasmi.
Walioikosa Nafasi ya Ajira
Kwa waombaji ambao majina yao hayapo kwenye orodha, wanatakiwa kutambua kuwa hawakufaulu au hawakupata nafasi, hivyo wanahimizwa kuendelea kuomba nafasi pindi zitakapotangazwa tena.
Jinsi ya Kupakua Orodha ya Majina
Kwa waliofaulu, bofya kiungo hapa chini ili kupakua PDF yenye majina ya walioitwa kazini TFS na TAWA: