MAJINA ya Walioitwa Kazini UTUMISHI 08/05/2025
Taarifa Kuhusu Waombaji Kazi Waliofaulu
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ametoa taarifa kwa waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kati ya tarehe 16 Juni 2024 na tarehe 5 Aprili 2025. Matokeo ya waombaji kazi waliofaulu usaili huo yameorodheshwa katika tangazo hili.
Orodha ya Wasailiwa na Uhamisho wa Vituo vya Kazi
Orodha ya majina ya waliofaulu pia inajumuisha baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye kanzidata kwa kada mbalimbali, ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana. Waombaji kazi wote waliofaulu usaili na kupangiwa vituo vya kazi watazipata BARUA za kupangiwa vituo vya kazi kupitia Akaunti zao za Ajira Portal, kwenye sehemu ya My Applications.
Jinsi ya Kupakua na Kutumia Barua za Kuitwa Kazini
Waombaji kazi wanatakiwa kupakua barua hizo, kuzichapisha na kwenda nazo kuripoti katika vituo vya kazi walivyopangiwa.