Majina Walioitwa Kwenye Usaili NEC 2024: Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ni chombo huru cha Serikali kilichoanzishwa mwaka 1993 chini ya Ibara ya 74(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Kulingana na Ibara ya 65 ya Katiba hiyo, Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge, na Madiwani hufanyika kila baada ya miaka mitano (5).
Tanzania inafuata mfumo wa uchaguzi wa “First Past The Post,” ambapo mgombea mwenye kura nyingi zaidi hutangazwa kuwa mshindi. Mfumo huu umeainishwa katika Ibara ya 41 (6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977, Kifungu cha 35F(8), na Kifungu cha 81(a) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, pamoja na Kifungu cha 82(a) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292.
NEC hutumia watendaji mbalimbali kusimamia shughuli za uandikishaji na uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Watendaji hawa ni pamoja na Waratibu wa Uchaguzi wa Mkoa, Maafisa Waandikishaji, Waandishi Wasaidizi, na Waendeshaji wa Vifaa vya BVR. Mawakala wa Uandikishaji wa Wapiga Kura pia hupewa nafasi ya kushiriki.
Kwa mujibu wa Kifungu cha 15A cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, na Kifungu cha 17A cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu vinaweza kuteua mawakala katika kila kituo cha uandikishaji. Mawakala hawa hufuatilia na kuhakikisha kuwa mchakato wa uboreshaji unazingatia sheria, kanuni, na maelekezo yaliyowekwa na NEC.
Katika mwaka 2024, NEC imetangaza orodha ya walioteuliwa kwa usaili ili kujaza nafasi mbalimbali zinazohusiana na mchakato wa uchaguzi. Katika makala hii, tunakupa orodha ya majina ya walioteuliwa kwa usaili na maelezo muhimu kuhusu maandalizi ya usaili na hatua za kuchukua baada ya usaili.
Orodha ya Majina Walioitwa Kwenye Usaili wa NEC 2024
Hapa chini tumekuwekea viungo vya kupakua majina ya walioteuliwa kwa usaili wa NEC 2024 kwa halmashauri mbalimbali. Kila kiungo kina maelezo kuhusu waombaji walioteuliwa, pamoja na tarehe, muda, na mahali pa kufanyia usaili. Tafadhali chagua halmashauri yako ili kupata maelezo zaidi na kuhakikisha umejiandaa vizuri kwa hatua inayofuata katika mchakato wa ajira.
Majina Walioitwa Kwenye Usaili Tume ya Uchaguzi (NEC
Majina ya Walioteuliwa Kwenye Usaili wa NEC 2024
Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Uchaguzi Nsimbo anawatangazia waombaji kazi walioomba nafasi za Mwandikishaji Msaidizi na Mwendesha BVR kufika kwenye usaili. Vituo vya usaili na maelezo mengine yanapatikana kwenye viunganishi vya kata hapa chini:
- Usaili Kata Ya Ibindi.Pdf
- Usaili Kata Ya Itenka.Pdf
- Usaili Kata Ya Kanoge.Pdf
- Usaili Kata Ya Kapalala.Pdf
- Usaili Kata Ya Katumba.Pdf
- Usaili Kata Ya Litapunga.Pdf
- Usaili Kata Ya Machimboni.Pdf
- Usaili Kata Ya Mtapenda.Pdf
- Usaili Kata Ya Nsimbo.Pdf
- Usaili Kata Ya Sitalike.Pdf
- Usaili Kata Ya Ugalla.Pdf
- Usaili Kata Ya Uruwira.Pdf
Leave a Comment