Michezo

Majeruhi ya Ayoub Lakred Yathibitishwa na Simba SC

Majeruhi ya Ayoub Lakred Yathibitishwa na Simba SC

Simba SC imetangaza kuwa kipa wao namba moja, Ayoub Lakred, amepata majeraha ya paja wakati wa kambi ya maandalizi nchini Misri kwa ajili ya msimu mpya wa mashindano ya 2024/2025.

Afisa habari wa Simba, Ahmed Ally, amesema, “Ni kweli Ayoub ameumia paja na atafanyiwa vipimo akirejea ili kujua kama atahitaji matibabu ya kawaida au upasuaji. Madaktari bado hawajajua muda atakaokuwa nje, lakini tutapata taarifa kamili mara tu vipimo vitakapokamilika.”

Kikosi cha Simba kinarejea nchini leo baada ya kambi ya wiki tatu nchini Misri.

Leave a Comment