Ajira Tanzania

Luteni Feki wa JWTZ Matatani Simiyu!

Luteni Feki wa JWTZ Matatani Simiyu!

Mwanamume mmoja anayefahamika kwa jina la Nchambi Nsungwa Mapanda, maarufu kama Emanuel Gangala (24), amefikishwa mahakamani mkoani Simiyu kwa makosa ya kughushi utambulisho na kujifanya afisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka wa serikali, Betrice Mboya, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Mkoa wa Simiyu, Alex Mtenga, mtuhumiwa anadaiwa kutenda kosa hilo mnamo Februari 14, 2025, katika eneo la Shule ya Sekondari Simiyu. Inadaiwa alijitambulisha kwa umma kama afisa wa JWTZ mwenye cheo cha Luteni, akiwahadaa watu kuwa anaweza kuwasaidia kujiunga na jeshi na idara ya usalama wa taifa.

Sheria inataja kuwa kitendo hicho ni kinyume na Kifungu cha 100(b) na Kifungu cha 35 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, Sura ya 16, kama ilivyorekebishwa mwaka 2022.

Mbali na hilo, shtaka la pili linamtuhumu mtuhumiwa kwa kosa la kuvaa sare rasmi za JWTZ bila ridhaa wala mamlaka, jambo ambalo pia ni kinyume cha sheria.

Kwa sasa, mtuhumiwa anasubiri hatua zaidi za kisheria baada ya kufikishwa mahakamani.

Leave a Comment