Ajira

KUITWA KWENYE USAILI SHIRIKA LA BIMA LA TAIFA NIC 17-10-2024

Tangazo La Kuitwa Kwenye Usaili Shirika La Bima La Taifa NIC 17-10-2024

SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb.Na.JA.9/259/01/B/40 16-10-2024
TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Shirika la Bima la Taifa
(NIC) anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa
kuanzia tarehe 21-10-2024 hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili
huo.Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-

  1. Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili muda na sehemu ambapo
    usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.
  2. Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask)
  3. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
  4. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga
    kura,Kitambulisho cha kazi,Kitambulisho cha Uraia, Hati ya kusafiria, Leseni ya Udereva au barua ya
    utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji unachotoka.
  5. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa,kidato cha IV, VI,
    Astashahada, Stashahada,Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za
    Mwombaji.
  6. Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hatiza
    matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA
    HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
  7. Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
  8. Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
  9. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na
    Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA)
  10. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi
    vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya
    tangazo husika.
  11. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti
    vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.
  12. Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba
    ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa iku ya usaili.

Kuitwa Kwenye Usaili Shirika La Bima La Taifa NIC

Leave a Comment