Michezo

Kikosi cha Simba Vs Telecom Egypt leo 28/07/2024

Kikosi cha Simba Vs Telecom Egypt leo 28/07/2024

Kikosi cha Simba Vs Telecom Egypt leo – Mechi ya Kirafiki

Kikosi cha Simba Vs Telecom Egypt leo 28072024
Kikosi cha Simba Vs Telecom Egypt leo 28072024

Leo, tarehe 28 Julai 2024, mashabiki wa soka watashuhudia mtanange wa kirafiki kati ya wekundu wa Msimbazi, Simba Sports Club, na timu ya Telecom Egypt. Mechi hii inatarajiwa kupigwa kwenye uwanja wa Mercure kuanzia saa 1 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Mchezo huu ni sehemu muhimu ya maandalizi ya klabu Simba kuelekea msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara unaotarajiwa kuanza tarehe 8 Agosti. Wekundu wa Msimbazi watakuwa wakijaribu wachezaji wao wapya waliosajiliwa pamoja na mbinu zao za ushindi dhidi ya Telecom Egypt kabla ya kukutana na wapinzani wao wa jadi, Yanga SC, kwenye mchezo wa ngao ya jamii.

Huu utakuwa mchezo wa pili wa kirafiki kwa Simba katika kipindi hiki cha maandalizi ambacho wapo katika kambi maalumu Misri. Katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya El-Qanah ya Misri, Simba ilionyesha uwezo mkubwa kwa kushinda magoli 3-0. Jean Charles Ahoua alifunga magoli mawili ya haraka katika dakika za mwanzo, huku Okejepha akifunga goli la tatu na la mwisho katika dakika za nyongeza.

Mashabiki wa soka nchini wanatarajia kwa hamu kuona jinsi Simba itakavyocheza dhidi ya Telecom Egypt. Je, wekundu wa Msimbazi wataendeleza wimbi lao la ushindi? Au Telecom Egypt itatoa upinzani mkali? Majibu ya maswali haya yatapatikana leo usiku kwenye uwanja wa Mercure. Hapa tutakuletea kikosi rasmi cha Simba Sc Vs Telecom Egypt mara baada ya kutangazwa na kocha wa Simba.

Kikosi cha Simba Vs Telecom Egypt leo 28/07/2024 – Mechi ya Kirafiki

Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids, anatarajiwa kutangaza kikosi chake rasmi kitakachoanza katika mtanange wa leo dhidi ya Telecom Egypt majira ya saa 12 jioni. Huku tukisubiri kwa hamu tangazo hilo, Habariform inakuletea utabiri wa kikosi kinachoweza kuanza kulingana na mwenendo wa mazoezi na mechi zilizopita.

Kikosi Cha Utabiri: Ally Salim (1) Shomari Kapombe (12) Mohamed Hussein (15) Karaboue Chamou (2) Che malone (20) Mzamiru Yassin (19) Yusuph Kagoma (21) Edwin Balua (16) Joshua Mutale (7) Jean Charles Ahoua (10) Freddy Michael (18).

Leave a Comment