Kikosi Cha Simba Vs APR 03 Agosti 2024 – Simba Day
Klabu ya Simba SC itakutana na APR ya Rwanda katika mchezo wa kirafiki kesho, 03 Agosti, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo kutakuwa na hafla ya kusherekea Simba Day 2024. Huu ni mchezo unaotarajiwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa Simba, kwani ni fursa ya kwanza kuona kikosi kipya kilichosajiliwa kwa ajili ya msimu ujao.
Kocha wa Simba, Fadlu Davids, ametamba kuwa baada ya wiki sita za maandalizi ya kujiandaa na msimu mpya, timu yake itakuwa moto wa kuotea mbali. Simba SC imerejea nchini baada ya kuweka kambi ya wiki tatu mjini Ismailia, Misri, ambako walicheza mechi tatu za kujipima nguvu na kushinda zote. Matokeo ya mechi hizo za kirafiki nchini Misri ni ushindi wa 3-0 dhidi ya El-Qanah, na ushindi wa 2-1 mara mbili dhidi ya Telecom Egypt na Al-Adalah FC ya Saudi Arabia.
Kikosi cha Simba Dhidi ya APR Mechi ya Kirafiki
Kocha Davids amesema usajili wa wachezaji 14 wapya pamoja na wachezaji 14 waliokuwepo umekamilisha kikosi chenye nguvu na nishati. Wachezaji wapya wameonyesha uelewa wa haraka wa mafunzo na mbinu zinazohitajika, jambo ambalo limeongeza ubora wa kikosi.
Kocha Fadlu Davids pia ameweka wazi kuwa maandalizi ya kikosi ni mchanganyiko wa mazoezi ya kimwili na mbinu za kiufundi.
“Mimi ni kocha ambaye siwezi kutofautisha ufiti na mbinu. Hivyo kuanzia siku ya kwanza tulianza kufanyia kazi maandalizi ya kimbinu na jinsi gani tunacheza,” alisema Fadlu.
Kocha huyo anatarajia kuona wachezaji wakiwa na staili ya kiuchezaji inayotakiwa kufikia mwisho wa mapumziko ya FIFA, na kuongeza kuwa kikosi chake kitakuwa na ushirikiano mzuri na mzunguko kamili wa maandalizi ya kimwili na ya kiufundi.
Kikosi Cha Simba Vs APR 03 Agosti 2024 – Simba Day 2024
Hiki apa kikosi cha Simba dhidi ya APR kilichotangazwa
- Salim
- Kapombe
- Hussein (C)
- Che Malone
- Chamou
- Ngoma
- Mutale
- Mzamiru
- Mukwala
- Ahoua
- Awesu
Wachezaji wa Ziada; Hussein, Camara, Hamza, Kijili, Duchu, Kazi, Nouma, Omary, Fernandez, Okeejepha, Karabaka, Chasambi, Baluu, Mashaka & Kibu
Leave a Comment