Simba Sports Club leo itakuwa na changamoto ya kupambana na Al Adalah FC katika mchezo wa tatu wa kirafiki kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2024/2025. Mchezo huu unatarajiwa kuanza majira ya saa moja usiku katika uwanja wa New Suez Canal, Misri.
Katika michezo miwili ya kirafiki ambayo wekundu wa Msimbazi wamecheza wakiwa katika kambi yao ya maandalizi nchini Misri, wameweza kushinda michezo yote. Katika mchezo wa kwanza dhidi ya El-Qanah, Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-0, na katika mchezo wa pili dhidi ya Telecom Egypt, walishinda kwa mabao 2-1.
Mechi ya leo dhidi ya Al Adalah FC inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa zaidi ikilinganishwa na michezo miwili ya kwanza kutokana na Al Adalah FC kuwa na wachezaji wenye viwango bora licha ya kuwa wanashiriki katika ligi daraja la kwanza Saudi Arabia. Katika mchezo huu, Simba SC inatarajiwa kuendeleza rekodi yake ya kutofungwa, hivyo tunatarajia kuona mbinu za kocha wa Simba, Faldu David.
Soma: Matokeo Simba Vs Al Adalah FC Leo – Mechi ya Kirafiki
Kikosi Cha Simba Dhidi ya Al Adalah FC Leo (29/07/2024) – Mechi ya Kirafiki Kocha mkuu wa Simba anatarajiwa kutangaza kikosi rasmi kitakachoanza katika mchezo wa leo dhidi ya Al Adalah FC saa moja kabla ya kipute kuanza, majira ya saa 12 jioni. Wakati tukisubiri kwa hamu kikosi kamili, tumekuandalia uchambuzi wa kina wa kikosi kinachoweza kuanza kwa Simba, tukizingatia uwezo na mchango wa wachezaji katika michezo iliyopita.
Kikosi Cha Simba Vs Al Adalah FC Leo
Hiki ndicho kikosi chetu cha utabiri:
- Hussein Abel
- David Kameta
- Valentin Nouma
- Hussein Kazi
- Abdulazak Hamza
- Augustine Okajepha
- Ladaki Chasambi
- Debora Fernandez
- Freddy Micanel
- Omary Omary
- Salen Karabaka
Leave a Comment