Mshambuliaji wa Simba, Kibu Denis, amepewa programu maalum ya mazoezi na Kocha Mkuu Fadlu Davids ili kuboresha utimamu wake. Kibu hakushiriki kambi ya Simba wakati wa pre-season kwani alikwenda Marekani kwa mapumziko na baadaye Ulaya kwa ajili ya kujiunga na timu moja ya Ligi Kuu ya Norway, lakini dili hilo halikufanikiwa na akarudi Simba.
Kibu Denis amepewa programu maalum
Fadlu Davids amesema, “Kwa kuzingatia utimamu wa kikosi changu, nimeona nimpe Kibu mazoezi tofauti ili kuwa imara zaidi na tayari kwa asilimia zote. Nina imani kubwa na mchezaji huyo anaweza akawa chachu ya ushindani kikosini, hasa eneo la ushambuliaji.”
“Tunahitaji wachezaji walio tayari kiushindani kabla ya kuingia katika michuano ya ligi ya ndani na kimataifa, hili nimelifanya kwa asilimia kubwa kwa wachezaji niliokuwa nao Misri,” aliongeza Fadlu.
Simba na Yanga zitakutana kesho katika mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Ngao ya Jamii, utakaofanyika kwenye Uwanja wa Mkapa majira ya saa 1:00 usiku.
Leave a Comment