Jinsi ya Kupika Tambi na Nyama ya Kusaga

0
Jinsi ya Kupika Tambi na Nyama ya Kusaga
Jinsi ya Kupika Tambi na Nyama ya Kusaga

Jinsi ya Kupika Tambi na Nyama ya Kusaga kwa Haraka na Ladha Bomba

Unatafuta mlo wa haraka, rahisi lakini una ladha tamu na ya kuvutia? Tambi na nyama ya kusaga ni mlo bora kwa wanafunzi, wafanyakazi, na watu wenye ratiba ngumu lakini wanapenda kupika chakula chao nyumbani.

Faida ya Pishi Hili

Pishi hili halihitaji muda mrefu kuandaa, lakini linakupa virutubisho kamili na ladha ya kipekee. Nyama ya kusaga huwa tayari imeandaliwa sokoni au madukani, jambo linalorahisisha zaidi maandalizi yako jikoni.

Mahitaji ya Kupika Tambi na Nyama ya Kusaga

  • Tambi (Spaghetti) – kiasi unachotaka
  • Nyama ya kusaga – kiasi cha kutosha
  • Kitunguu maji – kikubwa kimoja
  • Nyanya ya kopo – kidogo
  • Karoti – 1 au 2 kulingana na upendeleo
  • Pilipili hoho – kijani au nyekundu
  • Chumvi – kiasi
  • Simba mbili (curry powder)
  • Mafuta ya kupikia – kiasi

Hatua kwa Hatua Jinsi ya Kupika

1. Andaa Mboga

  • Menya na katakata kitunguu maji, karoti, na pilipili hoho vipande vidogo.
  • Viweke pembeni kwa matumizi ya baadaye.

2. Kaanga na Tayarisha Mchuzi wa Nyama

  • Weka sufuria jikoni, ongeza mafuta na usubiri yapate moto.
  • Ongeza kitunguu na kaanga hadi kibadilike rangi kuwa ya kahawia.
  • Weka nyanya ya kopo, endelea kukoroga hadi ichemke vizuri.
  • Ongeza curry powder (simba mbili) na chumvi, changanya vizuri.
  • Ongeza nyama ya kusaga, iache ichemke hadi iive vizuri.
  • Mwisho, ongeza karoti na pilipili hoho, acha ichemke kwa dakika 2, kisha ipua.

3. Pika Tambi

  • Katika sufuria nyingine, chemsha maji ya kutosha.
  • Ongeza chumvi, mafuta kidogo na tambi.
  • Zichemke hadi ziive, kisha zichuje maji yote kwa kutumia chujio.
  • Zirejeshe jikoni kwa moto mdogo kwa muda mfupi ili zikauke.

4. Tayari kwa Kuliwa

  • Panga tambi katika sahani, ongeza nyama ya kusaga juu yake au pembeni.
  • Unaweza kuzipamba na majani ya giligilani kwa ladha zaidi.

Ushauri wa Ziada

Pishi hili linaweza kuongezewa jibini (cheese) juu kwa wale wapendao ladha ya Kiitaliano. Pia, unaweza kutumia tambi za aina tofauti kulingana na upatikanaji.

Kwa siku zenye haraka, tambi na nyama ya kusaga ni suluhisho bora la chakula kitamu na kinachoshiba!

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here