Jinsi ya Kuhakiki Udahili wa Chuo NACTVET 2025

0
Jinsi ya Kuhakiki Udahili wa Chuo NACTVET 2025
Jinsi ya Kuhakiki Udahili wa Chuo NACTVET 2025

NACTVET: Jinsi ya Kuhakiki Udahili wa Vyuo kwa Mwaka 2025

Je, Umedahiliwa Katika Chuo cha Kati kwa Ngazi ya Astashahada au Stashahada?

Kama jibu ni ndiyo, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) linakukumbusha umuhimu wa kuhakiki udahili wako rasmi kwa kufuata hatua sahihi kupitia mfumo wao wa mtandaoni. Hii ni hatua muhimu ili kuhakikisha taarifa zako ziko sahihi kabla ya kuendelea na masomo au kupata nyaraka rasmi.

Hatua kwa Hatua: Jinsi ya Kuhakiki Udahili NACTVET

  1. Tembelea tovuti ya NACTVET: www.nactvet.go.tz
  2. Bofya kiungo kinachosema: “Student Information Verification
  3. Jaza taarifa zako kwa usahihi kama mfumo utakavyoelekeza
  4. Hakiki chuo ulichosajiliwa na programu unayosoma
  5. Ikiwa kuna changamoto yoyote, wasiliana na Afisa Udahili wa chuo chako
  6. Tembelea mfumo mara kwa mara kuhakiki taarifa zako na matokeo ya kila muhula
  7. Iwapo matokeo si sahihi, wasiliana na Afisa wa Mitihani wa chuo chako

Kumbuka Muhimu

Ukamilifu wa taarifa zako kwenye mfumo huu ndio utakaoamua:

  • Upatikanaji wa Namba ya Utambuzi wa Tuzo (AVN)
  • Kupata Hati rasmi ya Matokeo (Transcript) baada ya kuhitimu

Ni muhimu kuhakikisha taarifa zako zote ziko sahihi ili kuepuka matatizo ya baadaye katika utoaji wa vyeti au uhamisho wa masomo.

Huduma kwa Wateja

Kwa msaada au maelezo zaidi, piga bure kupitia namba rasmi ya NACTVET:

📞 0800 110 388

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here