Michezo

Jeuri ya Kibu Denis Kuondoka Simba Inatokana na Kipengele Hiki

Jeuri ya Kibu Denis Kuondoka Simba Inatokana na Kipengele Hiki

Kibu Denis ana uhakika wa kuondoka Simba SC kutokana na kipengele maalum kwenye mkataba wake kinachomruhusu kuhamia Ulaya. Kipengele hiki kinampa jeuri ya kuondoka klabuni hapo wakati wowote atakapopata nafasi ya kucheza Ulaya.

Klabu ya Kristiansund BK tayari imewasiliana rasmi na Simba SC ikitaka kumnunua mchezaji huyo kwa kuzingatia kipengele hicho cha mkataba.

Akizungumza na kituo cha Crown fm, Kibu alikana madai ya Rashid Yazidi aliyekuwa akidai kuwa msimamizi wake. Kibu alifafanua kuwa Rashid hakuwa meneja wake bali alikuwa tu mwanasheria aliyempa kazi ya muda mfupi.

“Rashid sio meneja wangu, nilimpa kazi kama mwanasheria lakini hakuwa mwanasheria wangu. Tulimalizana na hana madai yoyote kwangu. Wakala wangu halisi ni Carlos Mastermind,” alisema Kibu Denis Prosper.

Leave a Comment