Michezo

Imani Kajula Amkaribisha Bosi Mpya Simba

Imani Kajula Amkaribisha Bosi Mpya Simba

Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Imani Kajula, amempokea rasmi Afisa Mtendaji Mkuu mteule, Uwayezu Francois Regis. Katika mazungumzo yao, Kajula alimpatia Regis ufahamu kuhusu mikakati mbalimbali endelevu ya klabu.

Kajula alimjulisha Regis masuala muhimu yanayohusu utendaji kazi wa klabu, mifumo yake, wadau, na mipango ya baadaye. Hii ni sehemu ya mchakato wa kuhakikisha uongozi mpya unaendelea bila matatizo.

Imani Kajula amkaribisha rasmi Uwayezu Francois Regis
Imani Kajula amkaribisha rasmi Uwayezu Francois Regis

Umma ulifahamishwa awali kuwa Kajula ataendelea kumsaidia Regis hadi Agosti 31, 2024. Baada ya hapo, Kajula ataondoka rasmi na Regis atachukua majukumu kama Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba.

Imani Kajula amkaribisha rasmi Uwayezu Francois Regis

Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Imani Kajula akiongea na Afisa Mtendaji Mkuu mteule, Uwayezu Francois Regis baada ya kumkaribisha.

Pamoja na kumpitisha kwenye masuala kadhaa kuhusu klabu alimpa maelezo ya kina juu ya mikakati mbalimbali endelevu.

Kama ambavyo umma ulijulishwa hapo awali, Kajula ataendelea kumpatia Regis uwelewa wa mifumo, utendaji kazi , wadau, mikakati na masuala mengine ya klabu hadi Agosti 31, 2024, ambapo Kajula ataondoka rasmi na Regis kushika hatamu ya kazi za Afisa Mtendaji Mkuu.

Leave a Comment