Ngao ya Jamii ni moja ya mashindano yanayovuta hisia nyingi katika soka la Tanzania, ikifungua msimu mpya wa ligi kwa mtanange mkali kati ya klabu bora za msimu uliopita. Mashindano haya yalianzishwa mwaka 2001 kwa lengo la kuleta mshikamano na furaha kwa mashabiki wa soka nchini.
Mwanzo wa Ngao ya Jamii
Ngao ya Jamii ilianza rasmi mwaka 2001 kwa mechi kali kati ya watani wa jadi, Simba na Yanga. Katika mchezo huo wa kihistoria, Yanga ilishinda kwa mabao 2-1, yaliyofungwa na Edibily Lunyamila na Ally Yussuph ‘Tigana’, huku bao pekee la Simba likifungwa na Steven Mapunda ‘Garincha’. Hata hivyo, mashindano haya hayakuendelea hadi mwaka 2009 yalipoanzishwa tena.
Orodha ya Washindi wa Ngao ya Jamii
Tangu kurejea mwaka 2009, Ngao ya Jamii imekuwa kipimo muhimu cha kuashiria mwanzo wa msimu mpya wa ligi kuu ya Tanzania. Hapa kuna orodha ya washindi wa Ngao ya Jamii miaka yote:
Mwaka | Mshindi | Matokeo |
---|---|---|
2001 | Yanga SC | 2-1 Simba SC |
2009 | Mtibwa Sugar | 1-0 Yanga SC |
2010 | Yanga SC | 3-1 Simba SC (Pen) |
2011 | Simba SC | 2-0 Yanga SC |
2012 | Simba SC | 3-2 Azam FC |
2013 | Yanga SC | 1-0 Azam FC |
2014 | Yanga SC | 3-0 Azam FC |
2015 | Yanga SC | 8-7 Azam FC (Pen) |
2016 | Azam FC | 4-1 Yanga SC (Pen) |
2017 | Simba SC | 5-4 Yanga SC (Pen) |
2018 | Simba SC | 2-1 Mtibwa Sugar |
2019 | Simba SC | 4-2 Azam FC |
2020 | Simba SC | 2-0 Namungo FC |
2021 | Yanga SC | 1-0 Simba SC |
2022 | Yanga SC | 2-1 Simba SC |
2023 | Simba SC | 3-1 Yanga SC (Pen) |
Mafanikio ya Simba na Yanga katika Ngao ya Jamii
Simba imefanikiwa kushinda Ngao ya Jamii mara kumi (10) tangu mwaka 2011 walipoifunga Yanga kwa mabao 2-0. Ushindi wao wa hivi karibuni ulikuwa mwaka 2023 dhidi ya Yanga kwa mikwaju ya penalti.
Kwa upande wa Yanga, wamechukua Ngao ya Jamii mara saba (7) tangu ushindi wao wa kwanza mwaka 2001. Ushindi wao wa hivi karibuni ulikuwa mwaka 2022 walipowashinda Simba kwa mabao 2-1.
Ushindani wa Ngao ya Jamii
Simba na Yanga ndizo klabu zinazotawala mashindano haya, zikileta burudani na ushindani mkubwa kwa mashabiki. Azam FC na Mtibwa Sugar pia zimeweza kujipatia ushindi kila moja mara moja, zikionyesha kuwa zina uwezo wa kushindana na vigogo wa soka nchini.
Leave a Comment