Hatua Muhimu za Kupata Leseni ya Biashara ya Duka la Rejareja
Katika mwaka 2024, kupata leseni ya biashara ni hatua muhimu kwa wafanyabiashara wa duka la rejareja. Leseni hii hutolewa na mamlaka husika kwa mujibu wa Sheria ya Leseni ya Biashara Na. 25 ya mwaka 1972 na marekebisho yake.
Makundi ya Leseni za Biashara
Leseni za biashara zimegawanywa katika makundi mawili:
- Kundi A: Leseni hizi ni kwa biashara zenye mtaji mkubwa kama vile wauzaji wa bidhaa nje ya nchi, huduma za mawasiliano, bima, na taasisi za fedha. Leseni hizi hutolewa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA).
- Kundi B: Leseni hizi hutolewa na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Zinajumuisha biashara kama migahawa, hoteli, vyama vya ushirika, na uuzaji wa bidhaa jumla na rejareja. Afisa Biashara wa Halmashauri ndiye anayetoa leseni hizi.
Mambo Muhimu katika Leseni ya Biashara
Leseni ya biashara inapaswa kuwa na:
- Namba ya leseni
- Aina ya leseni
- Jina la mamlaka iliyotoa leseni
- Namba ya mlipa kodi (TIN)
- Jina la kampuni au muombaji wa leseni
- Mahali biashara ilipo
- Kiasi cha ada kilicholipwa
- Namba ya stakabadhi na tarehe ya malipo
- Sahihi ya mtoaji wa leseni
- Jina na muhuri wa mamlaka husika
Leseni hii inalinda biashara yako na kukuepusha na usumbufu. Hakikisha unapata leseni kutoka mamlaka husika.
Vigezo vya Kupata Leseni ya Biashara
Muombaji anapaswa kujaza fomu ya maombi na kuambatanisha nyaraka zifuatazo:
- Hati ya kujiandikisha kama mlipa kodi (TIN)
- Cheti cha usajili wa kampuni
- Mkataba wa pango kama sehemu ya biashara umepanga
- Cheti cha uthibitisho wa mlipa kodi
- Vyeti vya kitaalamu kama inahitajika (mfano, TCRA kwa huduma za mawasiliano, TBS kwa huduma za chakula)
Namna ya Kufanya Malipo ya Ada ya Leseni ya Biashara
Malipo ya ada ya leseni hufanyika kupitia Mfumo wa Mapato ya Serikali za Mitaa. Mteja atapatiwa ankara na Afisa Biashara na kulipa fedha benki.
Kiwango cha Ada na Muda wa Matumizi ya Leseni
Ada ya leseni hutegemea aina ya biashara na hutofautiana kati ya maeneo mbalimbali. Leseni ya biashara hutumika kwa kipindi cha mwaka mmoja tangu ilipotolewa.
Faida ya Kuwa na Leseni ya Biashara
- Kutambulika kisheria
- Kusaidia kufungua akaunti ya biashara
- Kutumika kama nyaraka wakati wa kukopa
- Kuepuka usumbufu wa kufungiwa biashara
- Kukuza pato la taifa
Masharti ya Leseni ya Biashara
- Usitoe masharti yoyote kwa mnunuzi
- Toa risiti kwa mauzo yote
- Fuata sheria ya leseni ya biashara
- Uza bidhaa zinazokidhi viwango vya ubora
Leseni inaweza kunyang’anywa ikiwa ilipatikana kwa udanganyifu au ukiukaji wa masharti.
Leave a Comment