HomeMichezoGamondi Awachambua Simba SC Kabla ya Mechi

Gamondi Awachambua Simba SC Kabla ya Mechi

Gamondi Aeleza Faida za Maandalizi Kabla ya Mechi Dhidi ya Simba

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi, amesisitiza kuwa kuandaa kikosi chake kwa ufanisi ndio kipaumbele chake, badala ya kujishughulisha na wachezaji wapya wa Simba SC. Gamondi alisema hayo alipokuwa akizungumza na wanahabari kuelekea mechi ya Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba, itakayofanyika Dimba la Mkapa saa 1:00 jioni.

“Nimefanya kazi na wachezaji wangu mwaka mzima sasa, ingawa tumeongeza wachezaji wapya saba. Kwa Fadlu, ni kocha mpya na ana kikosi kipya, hivyo atalazimika kuwajua wachezaji wake wote vizuri kabla ya mechi ya Dabi,” alisema Gamondi.

Kocha huyo aliongeza kuwa hali hiyo inaweza kuwa faida kwake, lakini haimanishi kwamba ni sababu ya kushinda mchezo huo. “Soka ni mchezo wa makosa, na wakati mwingine mashabiki hawaelewi hilo, wanachotaka ni matokeo tu,” alihitimisha Gamondi.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Latest Posts