Michezo

Gamondi Ampa Onyo Nabi Sauzi

Gamondi Ampa Onyo Nabi Sauzi

Kocha wa Yanga Afunguka Kuhusu Safari ya Afrika Kusini

Miguel Gamondi, Kocha Mkuu wa Young Africans SC, amesema kuwa safari ya timu hiyo kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya msimu ni hatua muhimu katika kuitangaza klabu.

Gamondi alieleza hayo jana, Julai 26, 2024, wakati timu yake ikiwa bado ipo Afrika Kusini ikijiandaa kucheza dhidi ya Kaizer Chiefs, timu inayofundishwa na aliyekuwa kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi. Mechi hiyo inatarajiwa kufanyika kesho Jumapili, Julai 28, 2024, katika mashindano ya Toyota Cup.

“Ujio wetu hapa Afrika Kusini ni muhimu sana kwetu kwenye maandalizi ya msimu mpya wa 2024/25,” alisema Gamondi. “Kucheza na timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga) ni sehemu ya kuendelea kuitangaza klabu yetu barani Afrika na duniani kote.”

“Mchezo wetu dhidi ya Kaizer Chiefs utakuwa mzuri na wenye ushindani mkubwa, hasa ukizingatia Chiefs wana kocha mpya. Kila mchezaji atapata nafasi ya kumuonesha kocha uwezo wake, na kwa upande wetu maandalizi yetu yanazidi kuimarika. Tunaamini tutakuwa na mechi nzuri,” alisema Gamondi.

Mpaka sasa, Young Africans ikiwa Afrika Kusini, imecheza mechi mbili za Mpumalanga Cup dhidi ya FC Augsburg, timu inayoshiriki Ligi Kuu Ujerumani ‘Bundesliga,’ ambapo walipoteza kwa mabao 2-1, na kisha wakaifunga TS Galaxy bao 1-0.

Leave a Comment