Michezo

Fredy Michael Atabiriwa Kuwa Mfungaji Bora Simba

Fredy Michael Atabiriwa Kuwa Mfungaji Bora Simba

Fredy Michael ndiye atakayekuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Mshambuliaji wa Simba, Fredy Michael, amepewa nafasi kubwa ya kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu ujao. Wakati huo huo, Kibu Denis amepewa msamaha na mashabiki wa Msimbazi baada ya kutojiunga na kambi ya timu hiyo iliyofanyika Misri.

Kibu alipewa likizo na uongozi wa timu, akaenda Marekani kwa mapumziko kabla ya kurejea nchini na kwenda Norway kwa mazungumzo na timu moja bila idhini ya waajiri wake.

Leo, katika kilele cha tamasha la ‘Simba Day,’ Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally, alieleza kuwa hakuna shaka kuwa Fredy Michael atakuwa mfungaji bora wa msimu ujao. “Haina ubishi, bila shida yoyote, huyu ndiye mfungaji bora msimu huu,” alisema Ahmed.

Wakati huo huo, Ahmed alisema mashabiki wa Simba wamemsamehe Kibu kwa utovu wa nidhamu aliouonyesha kwa kutojiunga na kambi. “Sisi kama mashabiki tumekusamehe… ndugu wakigombana shika jembe ukalime, tumemaliza ugomvi na msimu huu bado yupo sana,” aliongeza Ahmed.

Leave a Comment