FERNANDES MAVAMBO APEWA MZIGO MKUBWA SIMBA
Debora Fernandes Mavambo amepokea changamoto kubwa kutokana na jezi atakayoivaa, namba 17, ambayo iliweka rekodi ndani ya kikosi cha Simba chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids.
Jezi hiyo maarufu ilivaliwa na Clatous Chama, ambaye sasa amehamia Yanga lakini bado anavaa jezi hiyo huko. Chama akiwa Simba aliisaidia timu kutwaa mataji mengi ikiwemo Ubingwa wa Ligi Kuu mara 4, FA mara 2, Mapinduzi mara 2, Ngao ya Jamii mara 2, na kuifikisha Simba hatua ya robo fainali Klabu Bingwa mara 4 na Kombe la Shirikisho mara 1.
Mavambo, licha ya presha ya kuvaa jezi hiyo, alijitambulisha vyema kwenye mechi ya kwanza ya Simba Day kwa kufunga bao moja kwenye ushindi wa 2-0. Alipiga shuti kali nje ya eneo la 18 na kufunga, akivutia wapenzi na mashabiki wa Simba kwa aina yake ya uchezaji.
Mavambo ni mchezaji mwenye uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya moja, akitumikia kama kiungo wa chini, kiungo mshambuliaji na kiungo mchezeshaji. Swali linalobaki ni kama ataweza kuitendea haki jezi namba 17. Muda pekee ndio utakaotoa jibu.
Leave a Comment