Michezo

Fei Toto Akosa Nafasi Kaizer Chiefs na Mamelodi

Fei Toto Akosa Nafasi Kaizer Chiefs na Mamelodi

Hali ya mchezaji wa Azam, Feisal Salum Abdallah, maarufu kama Fei Toto, imeshindwa kumwezesha kujiunga na timu kubwa za Afrika kama Mamelodi Sundowns na Kaizer Chiefs kutokana na masharti magumu yaliyo katika mkataba wake na Yanga.

Katika makubaliano yaliyowekwa kati ya klabu ya Yanga na Azam, iliamuliwa kuwa endapo Fei Toto atauzwa kutoka Azam kwenda timu nyingine yoyote, basi Azam inatakiwa kulipa Yanga shilingi bilioni 1 za Kitanzania. Hili limefanya kuwa vigumu kwa Fei Toto kuuzwa, kwani bei yake inaanzia bilioni 1.

Timu kadhaa maarufu, zikiwemo Mamelodi Sundowns na Kaizer Chiefs, zilionyesha nia ya kumsajili mchezaji huyo kutoka Zanzibar, lakini walipoelezwa kuhusu bei hiyo, walishangaa sana.

Inapaswa kufahamika kwamba Azam hawaitaji bei kubwa kwa hiari yao, bali ni kutokana na masharti ya mkataba ambao unawafunga hadi pale miaka mitatu itakapopita.

Leave a Comment