Michezo

Dodoma Jiji Vs Simba Sc: Matokeo na Magoli

Dodoma Jiji Vs Simba Sc

Mechi ya Dodoma Jiji Vs Simba Sc Leo 29/09/2024

Leo tarehe 29 Septemba 2024, mashabiki wa soka watashuhudia pambano kali kati ya timu ya Dodoma Jiji na Simba SC kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma. Mchezo huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara unatarajiwa kuanza majira ya saa 12:30 jioni, huku kila timu ikihitaji alama tatu muhimu kwa malengo yao tofauti msimu huu. Kwa Simba SC, ushindi utaiweka kwenye nafasi nzuri kuongoza msimamo wa ligi, huku Dodoma Jiji ikiwania ushindi wake wa kwanza baada ya mfululizo wa sare.

Matokeo ya Simba Sc vs Dodoma Jiji Leo

Dodoma JijiVSSimba Sc

Wekundu wa msimbazi Simba SC wameanza msimu wa 2024/2025 kwa kasi kubwa baada ya kushinda mechi zake zote tatu za awali. Kitu kinachoongeza ushindani kwa mechi hii ni kuwa Simba imekuwa na rekodi nzuri dhidi ya Dodoma Jiji, kwani katika michezo nane ya awali waliyokutana, Simba imeibuka mshindi katika kila mechi. Hii inawapa Simba SC matumaini makubwa ya kuendelea na rekodi hiyo nzuri.

Dodoma Jiji Vs Simba Sc

Kwa upande mwingine, Dodoma Jiji imekuwa na mwanzo wa msimu wenye changamoto, ikiwa imetoka sare katika michezo miwili mfululizo na kushinda mechi moja pekee kati ya nne walizocheza. Matokeo haya yanawafanya wenyeji kuhitaji ushindi leo ili kujiondoa kwenye mkwamo wa matokeo ya sare na kujiweka kwenye nafasi bora zaidi kwenye msimamo wa ligi.

Soma: Kikosi cha Simba Sc vs Dodoma Jiji Leo 29/09/2024

Kauli za Wachezaji Kuelekea Mchezo Huu

Straika wa Dodoma Jiji, Waziri Junior, amesema kuwa wamejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo huu na wanaingia dimbani kwa kujiamini. Alieleza kuwa kocha amewapa mbinu sahihi za kuwakabili Simba, na anaamini timu yao inaweza kupata matokeo mazuri, licha ya changamoto wanazokutana nazo. Waziri alisema: “Kocha ametuambia tuingie kwa kujiamini na kutumia nafasi zote tutakazopata, si rahisi kwa Simba kutoboa kwetu.”

Aidha, Ibrahim Ajibu ameongeza kuwa, mechi dhidi ya Simba haina utofauti mkubwa na mechi zingine walizocheza, ila wakiingia kwa heshima wakitambua ukubwa wa wapinzani wao. “Simba ni timu yenye mashabiki wengi, lakini tumejiandaa kuhimili presha hiyo na kufanya vizuri katika mchezo huu,” alisema Ajibu.

Leave a Comment