Michezo

Djigui Diarra Ashinda Tuzo Kipa Bora

Djigui Diarra Ashinda Tuzo Kipa Bora

Mlinda mlango wa klabu ya Yanga Sc, Djigui Diarra ameshinda tuzo ya golikipa bora wa Michuano ya FA (CRDB FEDERATION CUP).

Diarra amewashinda Khomein Abubakar kutoka Ihefu (Singida Black Stars) na Mohamed Mustafa kutoka Azam Fc.

Katika mashindano hayo Yanga ilitwaa Kombe hilo kwa mara ya tatu mfululizo, huku Diarra akiwa na msaada mkubwa kwa timu hiyo.

Djigui Diarra tangu atue Yanga amekuwa na kiwango bora na kuwa kiongozi kwa wachezaji wenzake pindi wanapokuwa uwanjani.

Uwezo wake wa kuanzisha mashambulizi kuanzia nyuma ya goli, umekuwa ukiisaidia timu hiyo kunufaika kitakwimu kwa kuongeza idadi ya wachezaji kwenye eneo la kiungo na ushambuliaji.

Timu nyingi kwa sasa duniani zinahitaji aina ya makipa kama Djigui Diarra wa Yanga.

Leave a Comment