Hans Rafael wa Crown Media ametoa tathmini ya kiungo mpya wa Simba, Debora Fernandes Mavambo, akieleza kwa kina uwezo wake wa kucheza. Rafael anasema Fernandes, anayefahamika kwa jina la utani “Midfield Dynamo,” ni mchezaji muhimu sana kwa Simba SC.
Mavambo amesifiwa kwa kuwa na umbo thabiti, unyumbulifu wa hali ya juu, na ustadi wa kupiga pasi sahihi. Hata hivyo, Fernandes anajulikana kwa mtindo wa soka wa haraka, akipendelea kupokea mpira na kuachia mara moja, hivyo kufanya iwe vigumu kumkaba. Ingawa bado hajaweza kucheza kwa dakika zote tisini, uwezo wake umeonekana katika mechi mbili alizocheza na Simba, na Rafael anaamini kwamba atakuwa mchezaji muhimu kuelekea msimu ujao.
Leave a Comment