HomeMichezoClement Mzize Awajibu Wakosoaji: "Naumia Kukosa Nafasi"

Clement Mzize Awajibu Wakosoaji: “Naumia Kukosa Nafasi”

Clement Mzize Awajibu Wakosoaji

Baada ya mjadala mkali sana kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mshambuliaji wa Yanga, Clement Mzize, kutotumia vizuri nafasi anazopata, mchezaji huyo amezungumza na kuwanyamazisha mashabiki wake. Mzize amekuwa Yanga kwa misimu mitatu sasa, akiwa tumaini kubwa la Wanayanga baada ya Fiston Mayele kujiunga na Pyramids FC ya Misri.

Msimu uliopita, Yanga ilifanikiwa kutoa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya NBC, Aziz Ki, lakini Mzize amekuwa akilaumiwa kila siku. Mchezaji huyo ameeleza jinsi hali hiyo inavyomtesa na jinsi alivyoipokea huku akiahidi kufanya vizuri zaidi katika msimu ujao wa 2024/25.

“Maneno ni mengi kuhusu mimi hasa nikikosa nafasi ya kufunga. Mimi pia naumia, lakini napata nguvu kutoka kwa kocha Gamondi ambaye siku zote amekuwa akiniambia mimi ni bora na natakiwa kuonyesha uwezo wangu. Licha ya maneno yake, ameendelea kunipa nafasi,” alisema Mzize na kuongeza, “Nafikiri kuendelea kuaminiwa na kupewa nafasi ndio siri ya mafanikio.”

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Latest Posts