Biashara

Bei ya Tiketi za Treni Ya Mwendokasi SGR 2024

Bei ya Tiketi za Treni Ya Mwendokasi SGR 2024

Bei ya Tiketi za Treni Ya Mwendokasi SGR, Nauli za Treni ya Mwendokasi Dar es salaam Kwenda Dodoma 2024

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imetangaza rasmi nauli za safari za treni ya mwendokasi ya SGR, na habari njema kwa wasafiri wote nchini ni kwamba bei za nauli sio kubwa kama wengi walivotarajia.

Nauli ya safari kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma, ambayo ni safari ndefu zaidi, ni Tsh 31,000 kwa watu wazima. Watoto wenye umri wa miaka 12 na chini wanapata punguzo kubwa, wakilipa nusu ya bei hiyo.

Je, unaelekea Makutupora? Hakuna shaka! Safari kutoka Dodoma hadi Makutupora inagharimu Tsh 37,000 kwa watu wazima, huku watoto wakiendelea kufurahia punguzo la asilimia 50.

Na kwa familia zinazosafiri na watoto wadogo, kuna habari njema zaidi: watoto chini ya miaka minne watasafiri bure kabisa!

LATRA imeweka nauli hizi kwa kuzingatia umbali wa safari, hivyo kuhakikisha kuwa wasafiri wanalipa kiwango cha haki kulingana na umbali wanaosafiri. Nauli hizi zina ushindani mkubwa ukilinganisha na mabasi yaendayo Dodoma, ambayo kwa kawaida hutoza kati ya Tsh 29,000 na Tsh 35,000. Kwa hivyo, SGR haitoi tu safari ya haraka na ya starehe bali pia ni chaguo la kiuchumi kwa wasafiri wengi.

Bei ya Tiketi za Treni Ya Mwendokasi SGR 2024

Nauli za Treni ya mwendokasi zimewekwa kwa kuzingatia umbali wa safari usika na umri wa abiria. Kwa watu wazima na watoto wenye umri zaidi ya miaka 12, bei ya tiketi imetajwa kuwa ni Tsh. 69.51 kwa kila kilomita. Watoto wenye umri kati ya miaka 4 na 12 watalipa nusu ya bei hiyo, yaani Tsh. 34.76 kwa kilomita. Watoto chini ya miaka minne watasafiri bure, lakini taarifa zao zitahitajika kurekodiwa.

Bei ya Tiketi Treni ya Mwendokasi SGR 2024 Kwa Abiria Wenye umri zaidi ya miaka 12

Bei ya Tiketi za Treni Ya Mwendokasi kwa daraja la kawaida kulingana na umbali wa vituo kuanzia Dar es Salaam hadi Makutupora kwa watu wazima na watoto wenye umri zaidi ya miaka 12 ni kama ifuatavyo;

Safari Umbali (Km)Nauli (Shilingi)
KutokaKwendaDaraja la Kawaida
Dar es SalaamPugu191000
Dar es SalaamSoga514000
Dar es SalaamRuvu735000
Dar es SalaamNgerengere134.59000
Dar es SalaamMorogoro19213000
Dar es SalaamMkata22916000
Dar es SalaamKilosa26518000
Dar es SalaamKidete31222000
Dar es SalaamGulwe354.725000
Dar es SalaamIgandu387.527000
Dar es SalaamDodoma44431000
Dar es SalaamBahi501.635000
Dar es SalaamMakutupora53137000

Bei Ya Tiketi Kwa Abiria Wenye umri Kuanzaia Miaka 4 hadi 12

Aidha, mchanganuo wa Bei ya tiketi za Treni ya mwendokasi kwa daraja la kawaida kulingana na umbali wa vituo kuanzia Dar es Salaam hadi Makutupora kwa watoto wenye umri kuanzia miaka minne (4) hadi 12 ni kama ifuatavyo;

SafariUmbali (Km)Nauli (Shilingi)
KutokaKwendaDaraja la Kawaida
Dar es SalaamPugu19500
Dar es SalaamSoga512000
Dar es SalaamRuvu732500
Dar es SalaamNgerengere134.54500
Dar es SalaamMorogoro1926500
Dar es SalaamMkata2298000
Dar es SalaamKilosa2659000
Dar es SalaamKidete31211000
Dar es SalaamGulwe354.712500
Dar es SalaamIgandu387.513500
Dar es SalaamDodoma44415500
Dar es SalaamBahi501.617500
Dar es SalaamMakutupora53118500

Leave a Comment