Bei ya King’amuzi Cha Azam
King’amuzi cha Azam TV na Bei Zake 2025
Azam TV imeendelea kuwa chaguo bora kwa Watanzania wengi kutokana na gharama nafuu na huduma bora za burudani. King’amuzi cha Azam kinawawezesha watazamaji kufurahia vipindi mbalimbali vya habari, michezo, filamu, tamthilia na muziki kwa gharama nafuu zaidi ukilinganisha na ving’amuzi vingine kama DStv na Zuku.
Kwa mwaka 2025, bei za ving’amuzi vya Azam TV vimebaki kuwa rafiki kwa wateja, huku ikitoa machaguo mawili makuu: king’amuzi cha Dish na king’amuzi cha Antena.
Bei za Ving’amuzi vya Azam TV 2025
Aina ya King’amuzi | Bei (TZS) | Maelezo |
---|---|---|
King’amuzi cha Dish | 99,000 | Kinakuja na dish, LNB, na nyaya. Hutoa chaneli nyingi za ndani na kimataifa, nyingi zikiwa katika ubora wa HD. |
King’amuzi cha Antena | 49,000 | Kinatumia mawimbi ya DVB-T2, hufaa kwa maeneo yenye mawimbi mazuri bila hitaji la dish. Hakihitaji malipo ya mwezi wa kwanza. |
Mahali pa Kununua King’amuzi cha Azam TV
Wateja wanaweza kununua king’amuzi cha Azam kutoka kwa mawakala rasmi wa Azam TV waliopo maeneo mbalimbali nchini Tanzania. Baadhi ya wauzaji maarufu ni:
- Dar es Salaam: Maranatha Electronics (Kariakoo), Kalam General Supplies (Gongo la Mboto)
- Mwanza: Yahya Mussa Faraji (Nyerere Road), Robbin Star Company LTD (Misungwi)
- Dodoma: Emmanuel Masila Matewa (Bahi Stendi)
- Arusha: Vunja Bei Electronics (Levolosi Street), Sunlight Power Supplies (Stand Kuu ya Zamani)
- Mikoa mingine: Mbeya, Morogoro, Tanga, Iringa, Mtwara, Kagera, na mikoa mingine nchini
Kwa orodha kamili ya mawakala walioidhinishwa, tembelea tovuti rasmi ya Azam TV au wasiliana na huduma kwa wateja kwa maelezo zaidi kupitia tovuti ya Azam TV.