Ballon d’Or 2025 Kufanyika Paris Septemba 22: Orodha ya Tuzo na Wanaowania
Hafla kubwa ya utoaji wa Tuzo za Ballon d’Or 2025 itafanyika Septemba 22, 2025, katika ukumbi maarufu wa Théâtre du Châtelet, jijini Paris, Ufaransa. Tukio hili litawakutanisha mastaa wakubwa wa soka duniani kuwania tuzo mbalimbali kutokana na mafanikio yao katika msimu uliopita.
Tuzo hizi ambazo zimekuwa zikitolewa tangu mwaka 1956 chini ya usimamizi wa jarida la France Football, mwaka huu zitaandikisha toleo la 69, zikidumisha heshima yake kama tuzo ya kifahari zaidi kwenye historia ya mchezo wa soka.
Tuzo Zitakazotolewa Ballon d’Or 2025
Katika hafla hiyo, tuzo zifuatazo zinatarajiwa kutolewa:
- Ballon d’Or – Mchezaji Bora wa Dunia (Wanaume)
- Ballon d’Or Féminin – Mchezaji Bora wa Dunia (Wanawake)
- Kopa Trophy – Mchezaji Bora Chipukizi
- Yashin Trophy – Kipa Bora kwa Wanaume na Wanawake
- Gerd Müller Trophy – Mfungaji Bora wa mwaka (Klabu na Taifa)
- Johan Cruyff Trophy – Kocha Bora wa Mwaka (Wanaume na Wanawake)
- Club of the Year – Klabu Bora ya Mwaka (Wanaume na Wanawake)
- Sócrates Award – Mchezaji mwenye mchango mkubwa kijamii
Wachezaji Wanaotajwa Kuwania Ballon d’Or 2025
Ingawa orodha rasmi ya wachezaji watakaowania tuzo hizo bado haijatolewa – inatarajiwa kutangazwa mapema mwezi Agosti – mashabiki na wachambuzi wa soka tayari wameanza kutaja majina yenye nafasi kubwa.
Baadhi ya wachezaji wanaopewa nafasi kubwa kuwania tuzo hizo kutokana na kiwango bora msimu huu ni:
- Kylian Mbappé
- Lamine Yamal
- Raphinha
- Ousmane Dembélé
Wachezaji hao wameonyesha ubora mkubwa kwenye ligi za ndani, michuano ya kimataifa, na mashindano ya bara mbalimbali.
Ballon d’Or 2025 inatarajiwa kuwa mojawapo ya matukio makubwa ya soka duniani mwaka huu, huku macho ya mashabiki yakielekezwa Paris kufuatilia nani ataibuka kidedea.
Leave a Comment