Tuzo ya Mfungaji Bora yaenda kwa Aziz Ki
Msimu wa 2023/24 ulikuwa wa mafanikio makubwa kwa Stephen Aziz Ki, akifunga mabao 21 katika Ligi Kuu Bara na kujinyakulia tuzo ya mfungaji bora. Aziz Ki ndiye aliyetawala orodha ya wafungaji wa ligi, akifunga mabao 21 kati ya 71 ya timu yake, Yanga, inayoongozwa na Kocha Mkuu Miguel Gamondi.
Kulingana na rekodi, Aziz Ki alifunga mabao 17 kwa mguu wa kushoto, matatu kwa mguu wa kulia, na moja kwa kichwa dhidi ya Tabora United katika Uwanja wa Mkapa. Katika eneo la penati, alifunga mabao 15, huku mabao sita akifunga nje ya eneo hilo. Aziz Ki alijulikana kwa uwezo wake mkubwa wa kupiga mipira huru, akitumia zaidi mguu wake wa kushoto.
Usiku wa Tuzo wa 2023/24 unatarajiwa kufanyika leo, Agosti Mosi 2024, Masaki. Wachezaji na viongozi watapewa tuzo, ikiwa ni maandalizi ya msimu mpya wa 2024/25.
Leave a Comment