Aziz Ki Ashinda Tuzo Tatu za TFF
Stephanie Aziz Ki, kiungo mshambuliaji wa Yanga SC, ameibuka kinara kwa kushinda tuzo ya mchezaji bora (MVP) wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara kwa msimu wa 2023/24. Aziz Ki ametwaa tuzo nne zenye hadhi, ikiwa ni pamoja na tuzo ya MVP, Kiungo Bora wa Ligi Kuu, Mfungaji Bora wa Ligi Kuu, na kuingia katika Kikosi Bora cha Msimu.
Pia, amemshinda Kipre Junior wa Azam FC na Feisal Salum ‘Feitoto’ wa Azam FC katika kipengele cha Kiungo Bora wa Ligi Kuu msimu huu. Kwa msimu uliopita, Aziz Ki alifunga magoli 21, akimpita mpinzani wake wa karibu, Feisal Salum, aliyefunga mabao 19.
Msimu huu, Yanga imeongeza wachezaji kadhaa wapya wenye vipaji vya hali ya juu, ambao huenda wakasaidia klabu hiyo kutwaa tuzo nyingi zaidi katika msimu mpya utakapoanza. Miongoni mwa maingizo mapya Yanga ni Clatous Chama, Chadrack Boka, Duke Abuya, Aziz Andabwile, Prince Dube, na Jean Baleke.
Leave a Comment