Michezo

Aziz Ki Aeleza Sababu za Kuikataa Kaizer Chiefs

Aziz Ki Aeleza Sababu za Kuikataa Kaizer Chiefs

Kiungo Bora Aziz Ki Aeleza Sababu za Kuikataa Kaizer Chiefs

Mchezaji wa Yanga na MVP wa Ligi Kuu ya Tanzania msimu uliopita, Stephane Aziz Ki, amefunguka kwa mara ya kwanza sababu za kuamua kubaki Yanga na kuzitupa ofa za timu nyingine.

“Najua Kaizer Chiefs na klabu zingine zinanihitaji, lakini pale mtu anapokuonesha heshima, wewe pia unatakiwa kurejesha heshima,” alisema Aziz Ki.

“Rais wa Yanga, Hersi Said, alikuja kuniona Berkane, nilipokuwa nacheza dhidi ya RS Berkane Morocco mwaka 2021. Baadaye walikuja kwa familia yangu kuongea nami mbele yao. Hii kwangu ilikuwa zaidi ya heshima. Unanitaka, pigia simu, sema Aziz nina ofa hii kwa ajili yako, lakini wao walikuja nyumbani.”

“Walitoka Dar es Salaam hadi kwa familia yangu. Hii kwangu ilikuwa heshima kubwa, wengine walikuwa wananipigia simu tu. Huwezi kupata watu kama Hersi. Ninathamini sana na nina furaha na mradi huu na jinsi ulivyokuja.”

“Yanga walinionyesha mradi wao, na mpaka sasa ninaamini katika mradi huo na ninaamini kwa Rais Hersi. Naweza kusema Hersi Said ni kama baba yangu. Naiona mradi unavyokwenda na kazi nzuri inayofanyika. Kwa sasa sio muda wa kuondoka Young Africans SC.”

Leave a Comment