Michezo

Alichosema Jembe Kuhusu Joshua Mutale

Alichosema Jembe Kuhusu Joshua Mutale

Mwandishi mashuhuri Saleh Ally Jembe ni miongoni mwa waliokuwa Misri kushuhudia maandalizi ya Simba kuelekea msimu wa Ligi Kuu Bara 2024/25. Jembe amezungumzia uwezo wa mchezaji mpya wa Simba, Mutale, akisema:

Kisukuma “Mutale” maana yake ni mkubwa, lakini hapa linahitaji kuvutwa kidogo. Huyu Mutale wa Simba, ingawa kiumbo si mkubwa, mambo yake ni makubwa sana na naamini atakuwa gumzo.

Ana kasi, nguvu, si mwoga, na ana uwezo wa kuwazidi hata walinzi watatu. Hatari zaidi ni kwamba ana uwezo wa kupiga mashuti makali sana.

Mfano mzuri ni bao la pili la Simba dhidi ya Wasaudi, ambapo alipokea mpira pembeni, akaenda kwa kasi na kupiga shuti kali lililogonga mwamba na kurudi ndani. Wakati walinzi wanajishauri, tayari alikuwa amefika tena na kupiga shuti la pili… BAO. Ninasema hili kwa sababu video ya bao hilo ninayo mimi peke yangu.

Kwa ujumla, ni mchezaji ambaye inaweza kuwa moja ya karata bora zilizopatikana na Simba na itachangia timu kurejea kwenye ubora wao.

Leave a Comment